Alhamisi 22 Januari 2026 - 01:30
Radi amali ya Ofisi ya Tabligh ya Hawza ya Qom Iran, kutokana na kauli za fedheha za Trump

Hawza/ Ofisi ya tabligh ya Hawza ya Qom, katika tamko kali, ililaani kauli za rais wa Marekani kuwa ni dharau dhidi ya matukufu ya Kishia na uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na ikasisitiza: Kauli hizi za kihuni hazitaathiri umoja wa Waislamu, bali kinyume chake, zitasababisha kuimarika zaidi kwa mshikamano wa watu na Wilaya na Marjaa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya tabligh ya Hawza ya Qom ilitoa tamko kulaani dharau za Trump dhidi ya hadhi ya Maraji' wa Kishia na uongozi wa Umma wa Kiislamu.

Maandishi ya tamko ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa midomo yao, lakini Mwenyezi Mungu atatimiza nuru Yake, hata kama makafiri watachukia.”
(Surat as-Saff, Aya ya 8)

Kufuatia kauli za fedheha, za kijinga na zilizojaa chuki za rais mchezaji kamari wa Marekani, ambaye kwa lengo la kudhoofisha misingi ya kiimani na kisiasa ya ulimwengu wa Kiislamu, amethubutu kudharau hadhi takatifu ya Maraji' wa Kishia na uongozi wa hekima wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma Imam Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu adumishe kivuli chake), Ofisi ya tabligh ya Hawza ya Qom inaeleza chuki na kulaani kwake kwa nguvu zote.

Kauli hizi zinatokana na kiwango cha juu cha kushindwa na kufilisika kwa mwanasiasa ambaye hana uelewa wa maslahi ya muda mrefu ya ulimwengu wa Kiislamu, na ambaye mbele ya wimbi la mwamko wa Kiislamu na ukubwa wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s), amekimbilia maneno ya hovyo na yasiyo na thamani. Maraji' wa Kishia ni uti wa mgongo wa kiroho na kiakili katika ulimwengu wa Kishia, wenye mizizi katika agano la Uimamu na uongofu wa Mwenyezi Mungu. Nafasi hii ni mrithi wa madhehebu ya kifiqhi na kiusuli ambayo daima imekuwa chanzo cha uongozi na mapambano dhidi ya uistikbari wa kimataifa. Kudharau uongozi na Maraji', kwa hakika ni kudharau Qur’ani, Ahlul-Bayt na misingi yote ya kidini inayoheshimiwa na kutukuzwa na mamilioni ya Waislamu duniani kote.

Uongozi wa Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (baraka zake zidumu) ni dhihirisho la kivitendo la kanuni ya Wilayat al-Faqih; kanuni ambayo ni dhamana ya uhuru na heshima ya Umma wa Kiislamu mbele ya njama za madola ya kimada na ya kidhalimu ya dunia. Yeye, kama mbeba bendera wa harakati ya Kiislamu, ni ngome imara mbele ya njama hizo.

Ofisi ya tabligh ya Hawza ya Qom inatangaza waziwazi kwamba: Aina yoyote ya matusi au dharau dhidi ya hadhi ya uongozi na Wilayat al-Faqih inachukuliwa kuwa ni shambulio dhidi ya malengo ya juu ya Mapinduzi ya Kiislamu na thamani za kiimani. Tukiwaunga mkono kwa nguvu Maraji' wa kidini na Uongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, tunawaambia wazi maadui wote kwamba kauli hizi za fedheha sio tu kwamba hazitadhoofisha azma na umoja wa Waislamu, bali kama ilivyokuwa hapo awali, zitaimarisha zaidi uhusiano wa watu na Wilaya na Marjaiya. Ulimwengu wa Kiislamu, kwa uelewa kamili, utazima juhudi hizi dhaifu na kuimarisha safu ya haki dhidi ya batili.

Na amani iwe juu ya wale wanaofuata uongofu.

Ofisi ya tabligh ya Hawza ya Qom

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha